
MOSHI SHABANI MALLEMA
Kufuatia kampeni zinazoendelea baadhi ya maeneo nchini ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na viongozi mbalimbali aidha kwa kufariki au sababu nyingine za kikanuni, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuwashawishi wanachama wa ACT Wazalendo na chama kikuu cha upinzani nchini cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA).

Katika kampeni zilizofanyika Kata ya Kijichi wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam CCM imefanikiwa kumpokea aliyekuwa mgombea udiwani katika kura za maoni ndani ya CHADEMA Rehema Holela ambaye aliambatana na wanachama wengine wasiopungua sita na kudai kutotendewa haki na chama hicho sababu iliyompelekea kuondoka na kumuunga mkono mgombea wa CCM Mama Tausi Milanzi kwani anaamini anaweza kuleta mabadiliko Kijichi kutokana na historia yake ya uchapakazi.

Kwa upande wa chama cha ACT Wazalendo kijana Johnson Ezra ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT kwa kata ya Kijichi naye amejiunga na CCM na kueleza kuwa chama cha ACT kimejaa ujanjaujanja na kimekosa muelekeo hivyo hakina dira thabiti ya kuiongoza Kijichi na Taifa kwa ujumla na kuwataka vijana wenzake kumchagua Mama Milanzi kwani atakuwa mlezi bora kwao kwa kuitekeleza ilani ya CCM ipasavyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida amewataka wanakijichi kuendelea kuwa na imani na CCM kwani imefanya makubwa kwa kipindi kichache na itaendelea kufanya hivyo, huku mgombea udiwani wa Kata hiyo akiwataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 22 ambayo itakuwa ni jumapili na wampigie kura za kutosha kwani anaimani anatosha na kueleza kuwa amekuwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo na alifanikiwa kuanzisha suala la VICOBA kwa kina mama, pia yeye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania kwa Kata ya Kijichi hiovyo anastahili kuchaguliwa na kuongeza kuwa kupitiq miradi itakayo fanyika Kijichi atahakikisha vijana wanapewa kipaumbele kwenye ajira na michezo, mikopo kwa wanawake na kuzisimamia kikamilifu pesa za mfuko wa maendeleo wa jamii TASAF zinawafikia wazee kama ilivyokusudiwa.


No comments:
Post a Comment