• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 20 January 2017

    Fella azidi kuwatafutia fursa Madada Sita

    Ukiachana na Jumba la Sanaa la Tanzania House of Talent liliotoa wakali kama Barnaba, Ditto, Linnah na wengine wengi wanaofanya vizuri kwasasa akiwemo Hitmaker wa Wangere maarufu kama Hamadai, Mkubwa na Wanawe chini ya uangalizi wa Mkubwa Fella au Said Fella ni sehemu mbayo kunavipaji lukuki na vyakilaaina
    Licha ya Yamoto Band iliyochini ya Mkubwa na Wanawe kufanya vizuri, Said Fella ameendele kuibua vipaji vipya na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana, hivi karibuni Fella aliwatambulisha Madada Sita katika ukumbi wa DAR LIVE wanaotamba na Wimbo wao wa Matobo na mapokezi yao yameonesha kuridhisha.
    Meya wa Halmashauri ya Temeke Abdallah Chaurembo akiwatunza Madada Sita katika hafla hiyo ya utiaji saini Mkataba daraja la Kijichi.
    Lakini hakuishia hapo ameendelea kuwatafutia fursa zaidi ambapo wamemeza kufanya show katika utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kijichi kati ya kampuni kutoka Korea ya CRJE na Halmashauri ya Temeke ambapo watu wengi walifurahishwa na show yao kiasi cha kuwaomba warudie tena.
    Licha ya Madada Sita, wasanii wengine kutoka Mkubwa na Wanawe waliotumbuiza kwenye hafla hiyo ni aliyekuwa mshindi wa Bongo Star Search maarufu kama Kayumba na mkali wa Singeli Dulla Makabila.
    Dulla Makabila Msanii wa Singeli kutoka Mkubwa na Wanawe
    Aliyekuwa Mshindi wa BSS Kayumba akitumbuiza katika hafla hiyo


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI