• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 20 January 2017

    DC Mjema na hapi wawatoa hofu wakazi wa DSM kuhusu uhaba wa chakula hii ndiyo hali halisi

    Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Salum Hapi amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula serikali na binafsi pamoja na masoko ili kujiridhisha na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
    Akizungumza mara baada ya ukaguzi alioufanya maeneo ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Kipawa NFRA, Ghala la Chakula na Nafaka Gongo Stores, Soko la Tandika, Soko la Buguruni, Soko la Tandale na Manzese kwa Msouth, Hapi amesema ameridhishwa na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kueleza kuwa chakula kipo cha kutosha ikiwemo mchele, mahindi, maharage na vile vyakula vyote vya kilimo cha kijani.
    Hivyo hakuna uhaba wa chakula na tetesi za njaa na uhaba wa chakula ni hadithi za kusadikika, alIsisitiza Hapi.
    Hapi amewataka wakazi wa Dar es Salaam waendelee na shughuli za uzalishaji kwani wafanyabiashara wote wamemuaminishia kuwa chakula kipo na hawana desturi ya kuficha chakula na mfanyabishara atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kosa la uhujumu uchumi na serikali itaendelea kuwaunga mkono.
    Pia kuhusu kamata kamata ya magari ya wafanyabishara amemuagiza Kamanda  wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Simon Siro kufuatilia suala na kuzitaka mamlaka zinazofanya hivyo kuacha mara moja, na wanaosambaza taarifa za uhaba wa chakula na njaa serikali itahakikisha inawashughulikia kwani wanaleta taharuki kwa wananchi.
    Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Mkoa wa Dar es Salaam Elizabeth Mashote ameeleza kuwa Dar es Salaam inatumia tani 2923 za chakula cha wanga kwa siku huku tani 530 zikiwa za vyakula vya protini na kusisitiza kuwa chakula kipo ila hofu iliyopo kuhusu suala la mvua na ukame ndiyo inapelekea bei kupanda na ukizingatia nchi ya Tanzania imeruhusu bishara huria hivyo haiwezi kuingilia suala la bei.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI