• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 20 January 2017

    Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, imepokea msaada wa meza kumi na moja na viti 11

    Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, leo Januari 19, 2017 imepokea msaada wa meza kumi na moja na viti 11 vyenye thamani ya dola za kimarekani 2647.52 kutoka kwa kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering Group Company.

    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Elisante Olle Gabriel amesema viti pamoja na meza hizo vitatumika katika ofisi za wizara ya habari zilizoko makao makuu ya nchi mjini Dodoma.

    "Tumepokea viti 11 na meza 11 kutoka kwa kampuni ya Jiangxi, lengo la kutupa msaada huu ni kusaidia safari ya kwenda Dodoma," amesema na kuongeza.

    "Msaada huu pia utasaidia kuimarisha na kujenga mahusiano baina ya nchi ya China na Tanzania."

    Mkurugenzi Mtendaji wa Jiangxi Geo-Engineering Group Company, Chen Yiang Hua amesema kampuni yake itaendelea kutoa msaada katika wizara hiyo hususan hiki ambacho wizara hiyo inatarajia kuhamia Dodoma.
    THU 6:04AM

    Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango leo amezindua jina jipya na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania (TPB) ambayo kuanzia leo  litatumika jina la TPB Bank Plc.

    Wakati akizungumza baada ya uzinduzi, Dkt. Mpango amesema serikali itaendelea kutoa msaada wa kifedha ili benki hiyo ijiimarishe kimtaji na kutekeleza majukumu yake.

    "Nimefarijika kusikia kuwa benki hii imefanikiwa kupeleka huduma zake za kibenki pembezoni mwa nchi, kujenga na kufungua matawi kwenye miji mikuu yote nchini," amesema.

    Dkt. Mpango ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Bank Plc kuhakikisha inapeleka gawiwo la serikali kwa wakati.

    "Benki yenu ihakikishe inaishawishi serikali kuendelea kuwekeza kwa kuipa gawiwo lake la faida kwa wakati na inavyostahili," 

    Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kubadilisha jina na nembo ni kwenda sambamba na mabadiliko ya kuiboresha benki. 

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Prof. Lettice Rutashobya alimhakikishia Dkt. Mpango kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwafikia watanzania wengi hasa walioko pembezoni ili waweze kunufaika na huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI