NAIBU Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Hamis Kigwangala, amezindua kifaa cha kupimia ugonjwa wa Selimundu ‘Sical Cell’, kinachotoa majibu ya haraka.
Akizindua kifaa hicho leo jijini Dar es Salaam, Kigwangala ameipongeza Kampuni ya Medomix Concept LTD kwa kusambaza , kifaa hicho hapa nchini kwani itasaidia sekta ya Afya kwa kiasi kikubwa.
Naipongeza sana hii kampuni ya Medomix Concept kwani, kifaa hicho hicho kitaweza kusaidia wagonja wengi kujulikana na mapema na ugonjwa wa huo wa Selimundu, ambao uonekana kwa mtu tangu akiwa mchanga’’, alisema.
Kigwangala alisema kuwa, uzuri wa kifaa hicho kinatoa majibua ya haraka ndani ya dakika 5 kinatoa majibu, hivyo utaondoa upungufu wa vifaa vya kupimia katika vituo vya hapa nchini, na kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika Hospitali za rufaa.
Aidha Kigwangala alisema dhamira ya Serikali ni kusambaza kifaa hicho katika vituo vya Afya vingi hapa nchini, ili kusaidia kuondoa mrundikano wa wagonjwa wanaopewa rufaa .
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Medomix Concept Bob Kabugi alisema kuwa, kifaa hicho kimekuwa msaada katika Hospitali nyingi nje ya nchini, hivyo wakaona wavilete na Tanzania, ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao.
‘’Kifaa hiki ni kizuri kwakuwa kinatoa majibu ya haraka, halafu hakitumii umeme, ni mchanganyiko wa damu ya mgonjwa na baadhi ya dawa, alafu unapata majibu ndani ya dakika 5, hivyo ni rahisi kwa matumiz’’, alisema
Kabugi alisema kuwa, kiko tayari kwa matumizi kwani tayari kimesajiliwa na Bodi ya maabara binafsi, hivyo kipo nchini kisheria.
No comments:
Post a Comment