• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 10 January 2017

    “MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AWAPA POLE WATU WALIOPOTEZA NDUGU ZAO KWENYE AJALI YA KUZAMA KWA JAHAZI BAHARI YA HINDI”

    poleMBUNGE wa
    Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku ametoa
    pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi
    kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya
    Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika
    kipindi hiki kigumu.
    Ajali ya
    Jahazi  ambayo
    ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria  12
    na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.
    Jahazi hilo
    lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani
    maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea
    Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na
    dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi  na
    kuzama
    Akizungumza na
    MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea
    kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na
    uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.
    Licha ya hivyo
    lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda
    12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo
    mbalimbali hapa nchini.
    Ajali hiyo
    ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye
    eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa
    kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.
    Alisema kuwa
    yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo
    nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali
    pema peponi.
     “Ajali sio jambo
    ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo
    vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani
    hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.
    Kamanda wa
    Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba
    alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na
    usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya
    hindi.
    Alisema kati
    ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa
    wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio
    hilo.
    Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado
    hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi
    eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.
    Kwa upande wake,
    Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
    Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na
    majeruhi 25.
    Alisema kati
    ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko
    watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na
    kuendelea na matibabu mengine

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI