kikosi cha Azam kwa ujumla bado hakifanyi vizuri kuanzia kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara pamoja na mechi mbili za kwanza za Kundi B kwenye michuano ya Mapinduzi ambapo ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Zimamoto kabla ya ‘kukaziwa’ na kulazimishwa suluhu na Jamhuri kwenye mechi yao ya pili.
Kiungo wa muda mrefu wa Azam Sure Boy anasema hayo yote yanasababishwa na ingizo la wachezaji wengi wapya na kuondoka kwa wachezaji wengi waliokuwa wamezoeana.
“Tumekuwa tunayumba kwenye michezo kadhaa kwa sababu ya ingizo la watu wengi wapya halafu timu nyingi za Zambia zinakamia.”
Abubakar ‘Salum Sure’ Boy ambaye alitangazwa Man of the match wa mechi ya Azam vs Yanga amesema Yanga ni timu kubwa na nzuri lakini makosa waliyofanya ndio yaliwapa wao mwanya wa kutumia nafasi za kufunga magoli.
“Yanga ni timu kubwa na tunajuana tunavyocheza ndio maana imekuwa hivi. Yanga timu yao nzuri mistake walizofanya sisi tumezitumia tukapata magoli, naamini Yanga wanatuogopa kila tunapokutana nao,” anasema Sure Boy ambaye alikuwa chachu ya ushindi wa Azam dhidi ya Yanga licha ya kutofunga goli hata mojal.
No comments:
Post a Comment