Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa
Wilaya ya Magharibi “A” akiweka saini kwenye kitabu cha wageni
alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwenye
Maonesho ya 53 ya Sherehe za Mapinduzi Zanzibar viwanja vya Miasara
Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Ndg.
Andrew W. Massawe akisaliana na Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman
mwananchi aliyetembelea banda la NIDA kupata huduma ya Usajili.
Ndg. Abdulaziz Juma Mtumwa
(kushoto) Afisa Msajili Msaidizi – NIDA akimsajili Ndg. Aboubakar
Mikidadi Othuman kupata kitambulisho cha Taifa baada ya kupokea maelezo
ya kina toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.
Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa
chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial akiweka saini kitabu cha
wageni alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya vitambulisho vya
Taifa Zanzibar
Mmoja wa wananchi akipata maelezo
ya kina kuhusu muonekano mpya wa Kitambulisho cha Taifa alipofika
kutembelea banda la NIDA Maisara – Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg.
Andrew W. Massawe akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi kwenye banda
la Mamlaka ya Vitambulisho NIDA- Maisara Zanzibar.
……………
Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar yameendelea leo kwenye viwanja vya Maisara –
Zanzibar, ambapo wananchi wameendelea kumiminika kwa wingi kwenye banda
la maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kusajiliwa, kuchukua
vitambulisho vyao na kupata elimu kuhusu umuhimu na faida za
Vitambulisho vya Taifa.
Miongozi mwa wageni waliotembelea
banda hilo ni Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”,
Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait
Memorial, ambao wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa na kupendekeza Vitambulisho vya Taifa kuanza
kutumika katika shughuli mbalimbali ili kupunguza utitiri wa
vitambulisho.
“Tuimarishe utendaji na tufanye
kazi kwa malengo na kwa kufanikisha utendaji kwa kuendelea kuwa karibu
zaidi na Serikali za Wilaya, Shehia na wananchi” alisisitiza Mkuu wa
Wilaya.
Aidha; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dr. Andrew W. Massawe naye
amejumuika na wananchi wa Zanzibar kwa kutembelea na kukagua shughuli
zinazofanyika kwenye banda la NIDA Maisara- Zanzibar na kushiriki
kuzungumza na kujibu hoja za wananchi wa Zanzibar walio kuwepo kwenye
banda la NIDA kupata huduma. Wananchi hao wameonyesha kufarijika na
utendaji wa Mkurugenzi huyo na kuelekeza furaha yao kwa jinsi
alivyojitoa na kushirikiana na wafanyakazi wake katika kujibu hoja
mbalimbali za wananchi.
Akizungumza wakati akijibu hoja za
wananchi, Bwana Masssawe amepongeza wananchi kujitokeza kwa wingi
kwenye banda la NIDA kupata huduma na ufafanuzi kuhusu Vitambulisho vya
Taifa; na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa
jumla kwa kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“NIDA tunaahidi kuendelea kuwa
karibu zaidi na wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri zaidi kwa
wananchi; lengo letu tuhakikishe kila Raia mwenye umri wa miaka 18 na
kuendelea anapata kitambulisho chake, pamoja na kuwasajili Wageni,
Wakimbizi wenye sifa za kuishi nchini kama sheria ya Usajili na Utambuzi
wa watu inavyoelekeza” Amesisitiza
Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar yalianza tarehe 07 Januari na yatamalizika
Jumamosi tarehe 14 Januari 2017 viwanja vya Maisara Zanzibar, NIDA ikiwa
miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwa kutoa huduma za Utambulisho kwa
wananchi na usawaji wa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha
taratibu za usajili
No comments:
Post a Comment