• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 13 January 2017

    MSUVA MFUNGAJI BORA MAPINDUZI CUP 2017

    Simon-Msuva-Yanga-Bongosoka
    Mshambuliaji hatari wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania,Simon Msuva ametetea tena kiatu chake cha ufungaji katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofikia Tamati hivi leo kwa klabu ya Azam FC kutwaa kombe hilo kwa kuifunga Simba.
    Msuva ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga jumla ya magoli manne baada ya kuyafunga katika hatua ya makundi ambapo timu yake ilikuwa kundi B.
    Licha ya kuchukua kiatu cha ufungaji Msuva alishindwa kuipeleka timu yake Fainali ya Michuano hiyo baada ya kuondoshwa kwa njia ya matuta na mahasimu wao Simba jumla ya magoli 4-2 kutokana na dakika 90 kumalizika bila ya kufungana.
    Msuva hii ni mara ya pili kuchukua tuzo hiyo baada ya mwaka jana kuchukua huku timu yake ikitolewa nje na timu ya URA kwa njia matuta katika robo Fainali kwa kufikisha magoli matano.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI