Na Ofisa habari Mufindi
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya
Makazi Mhe. Angelina Mabula amesema serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa
dhati kupunguza kwa asilimia kubwa kama si kuondosha kabisa kero ya
migogoro ya ardhi nchini ili kuondokana na malumbano yanayozikabiri jamii
nyingi hapa nchini.
Mh. Mabula ameyasema hayo mjini Mafinga wakati wa ziara ya
kikazi aliyofanya wilayuani humo akiwa na lengo la kukagua masuala
mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake sanjari na kusikiliza kero za wananchi
zinazohusiana na migogoro ya ardhi.
Amesema kwa muda mrefu jamii nyingi hapa nchini zimekuwa katika
migogoro ya kugombea ardhi, jambo ambalo linachochea mafarakano miongoni mwa
wananchi, hivyo serikali imejizatiti kuhakikisha inapunguza au kuondosha
kabisa migogoro iliyopo na akatoa rai kwa wakurugenzi wa halmshauri kuhakikisha
wanasimamia vema masuala ya ardhi ili kuzuia kuibuka kwa migogoro mipya.
Aidha, amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Mji wa Mafinga
kuhakikisha anarasimisha makazi ya wakazi wa kata ya Kinyanambo iliyopo mjini
Mafinga kwa kuhakikisha kuwa makazi yao yanapimwa na wanapatiwa hati
ili wamiliki maeneo yao kisheria ili waishi kwa kujiamini katika maeneo
yao lakini pia waweze kuzitumia hati hizo kama dhamana katika taasisi za
kifedha
No comments:
Post a Comment