Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Sylivia Lupembe akitoa utambulisho wa viongozi kutoka TEA na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli mpya za Mwalimu J. K. Nyerere Kampasi ya Mlimani unaodhaminiwa na TEA ambao utakaogharimu shilingi Mil. 496. Kutoka kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa UDSM Dkt. Saudin Mwakaje, Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima na Kaimu Meneja Miradi ya Elimu TEA Anne Mlimuka.
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima wakisaini mkataba huo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Prof. Rwekaza Mukandala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA Graceana Shirima wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kuusaini. Kulia ni Kaimu Meneja Miradi ya Elimu TEA, Anne Mlimuka.
Uongozi wa TEA na UDSM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli za Mwalimu J. K. Nyerere zinazojengwa kandokando ya barabara ya Sam Nujoma, Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………..
Na Lilian Lundo – MAELEZO
Mamlaka ya Elimu Tanzania Tanzania (TEA) imetiliana saini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkataba wa ujenzi wa uzio katika hosteli za Mwalimu J.K. Nyerere Kampasi ya Mlimani.
Mradi huo umedhaminiwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu (Education Fund) utakaogharimu jumla ya shilingi 496,646,868 hadi kukamika kwa ujenzi huo.
Mkataba huo umesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa utekelezaji mradi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Kwa upande wake Prof. Mukandala aliwashukuru TEA kwa msaada huo na kuongeza kuwa ujenzi wa uzio hizo ni suluhisho kubwa kwa wanafunzi watakaoishi katika eneo la kampasi hiyo.
Alisema kuwa uzio utasaidia kuimarisha usalama wa wanachuo na mali zao kutokana na kuwepo eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu unaotokana na stendi ya mabasi ya simu 2000 , maduka ya Mlimani City pamoja na viwanja hivyo kutumika kama njia ya mkato na vijiwe kwa watu wasio na kazi.
TEA tayari imefadhili miradi mbalimbali Chuo Kikuu cha UDSM ikiwemio ujenzi wa vyumba vya mihadhara, ununuzu wa vitabu vya kiada, vifaa kwa ajili ya wanafunzi kwenye mahitaji maalum, ufadhili wa kozi za “Pre Entry” kwa wanafunzi wa like katika masomo ya sayansi, ununuzi wa mitambo na vifaa vya Tehama.
No comments:
Post a Comment