Kwa kuliona hilo Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na
kutengeneza thamani ya Mwalimu na Taaluma ya ualimu (TEACHERS JUNCTION) imeweza kusajili walimu 1240 katika taasisi hiyo katika Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.
Akizungumza na wanahabari Meneja Miradi wa Taasisi hiyo Salum Njama amesema kuwa ili kumuandaa Mwalimu kukabiliana na Changamoto zote za taaluma hiyo wanawafuata walimu vyuoni kwa muelekeza vitu gani vya kuzingatia ili kuwa na ubora unaotakiwa.
"Tunawafuata hawa walimu wakiwa vyuoni ili kuzungumza nao na kuwaelekeza vitu muhimu vya kuzingatia akiwa chuoni ili vimtengeneze yeye kuwa mwalimu bora popote atakapo hitajika iwe Serikalini au shule binafsi".Alisema
"Aidha Njama ameishauri Serikali kutengeneza usimamizi mzuri kwa Taasisi zinazoendesha mafunzo ya ualimu kwani nyingi zimekuwa
zikifanya biashara bila kungalia ni aina gani ya Mwalimu anatengenezwa na Je, atakidhi vigezo.
No comments:
Post a Comment