..
Tuesday, 3 January 2017
Habari
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa ametoa siku Tatu kwa watumishi 10 ambao wamepewa uhamisho wa kazi toka wilaya Temeke kuripoti katika eneo la kazi katika manispaa ya Kigamboni haraka iwezekanavyo kabla hawaja chukuliwa hatua za kinidhamu.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo Leo katika ziara yake alipo kuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni , na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa kutembelea katika maeneo ya wananchi ili kutatua changamoto za wananchi.
Aidha Waziri Mkuu amefuta posho zote za kwa Halmashauri zote na ame elekeza fedha hizo kupelekwa katika shughuli za miradi ya Maendeleo , na ameongeza kuwa serikali imeunda tume kuchunguza mishahara ya watumishi ili waweze kuongezewa maslahi yao.
Pamoja na hayo Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali itaajiri walimu 4000 wa Masomo ya Sayansi na Hisabati ili kukabiriana na tatizo la upungufu wa walimu wa masomo hayo, na utaratibu unaendelea kufanywa baada ya kubaini watumishi hewa serikalini ile iweze kuanza kutoa Ajira.
Katika Hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ametembelea kiwanda cha Maziwa na Maji cha Watercom na Milkcom vilivyoko eneo la Kisarawe II na kuahidi kutatua changamoto zinakikabili kiwanda hicho ikiwemo miundombinu na kuiagiza mamlaka ya mkoa kushirikiana kikamilifu na sekta binafsi kama hiyo.
No comments:
Post a Comment