• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 5 February 2017

    Chama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia waitaka serikali kutokuchanganya maswala ya siasa na elimu



    Displaying IMG_9266.JPGChama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia waitaka serikali kutokuchanganya maswala ya  siasa na elimu kwakuwa anawaathiri wanafunzi .

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa miradi wa chama hicho Goodluck Moleli  amesema kuwa walimu wameonekana kutokushirikishwa katika maswala ya mabadiliko ya mitaala ya elimu na badala yake kutokujua mambo yanayo endelea  katika mabadiliko ya mitaala hiyo ya elimu.

    ‘’Leo hii tumekutana hapa katika warsha hii ya walimu iliyoandaliwa na Ceta ilikujadili ni jinsi gani ya kuboresha elimu ya Tanzania Lakini tunaiomba Serikali ipunguze maswala ya kubadilisha mitaala ya elimu mara kwa mara kwakuwa wanafunzi wengi wanashidwa kufanya vizuri katika masomo yao’’ amesema Moleli

    Mbali na hayo Mwalimu wa shule ya sekondari ya Kibweheri iliyopo Kibamba Sabrina Makafu amesema mtawala bado unashida na silabasi bado haziendani na vile tunavyo fundisha darasani mfano katika somo la kingereza unakuta tunacho fundisha sio kile kinacho toka katika mitihani.

    ‘’Inatupa sisi ugumu wa kufundisha kwakuwa tunayofunsisha hatuna uhakika kama ni hayo yatakayo letwa hivyo tunaiomba serikali kulifanyia kazi swala hili’’ amesema Mkafu.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI