Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Waganga
Wakuu wa Wilaya, Maafisa Maendeleo wa Jamii, Wanasheria, Madiwani na
Maafisa Mipango wa Halmashauri/Wilaya kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa
Dar Es Salaam Kinondoni Ilala na Temeke pamoja na Waandishi wa habari
waliopata fursa ya kushiriki wakati akifungua semina ya kupata mrejesho
wa maazimio kuhusu rasilimali zinazoboresha haki ya afya ya uzazi kwa
upande wa mamlaka za Halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam; na pia Kupata
mrejesho juu ya utekelezwaji wa maazimio yaliyowekwa na kila
Halmashauri/Wilaya kufuatia semina shirikishi iliyofanyika mwaka 2016
Mkoani hapa.Semina hiyo imefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini
Dar es salaam leo.
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya
Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akizungumza jambo wakati wa semina
hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
anayefuatia kwenye picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile pamoja na washiriki wengine wa semina hiyo.
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akifafanua jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile.
Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki
za wanawake na wanaume Mary Lusimbi ambaye ndiye alikuwa mwezeshaji wa
semina hiyo akitoa mada kwa washiriki wakati semina hiyo ilipokuwa
ikiendelea.
Bi. Halili Katani Afisa Ustawi wa
Jamii Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kulia
ni Balima Omari Afisa Maendeleo ya Jamii Manipaa ya Kinondoni na
katikati ni Tausi Kheri Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni
Baadhi ya washiriki waki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
Tausi Kheri Mwanasheria wa
Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kutoka kulia
ni Kheri Missinga Diwani Kata ya Bunju, Balima Omari Afisa Maendeleo ya
Jamii Manipaa ya Kinondoni na Kushoto ni Bi. Halili Katani Afisa Ustawi
wa Jamii Manispaa ya Kinondoni
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akifafanua
mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina
hiyo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment