Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku
uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano
Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo
Richard Muyungi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku
uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano
Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo
Richard Muyungi.
Picha na: Frank Mvungi – MAELEZO.
………………………………………………..
Na: Frank Shija – MAELEZO
SERIKALI imepiga rasmi marufuku
matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki
maarufu kama viroba kuanzia tarehe 1 Machi 2017.
Hayo yamebainishwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Januari Makamba wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
“Dhamira ya Serikali siyo kupiga
marufuku vinywaji vya pombe kali bali ni kutekeleza Ibara ya 14 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ambayo inatoa haki ya
kuishi katika mazingira yaliyo safi, salama na yenye afya,” alisema
Makamba.
Aliongeza kuwa uamuzi huo
wakusitisha matumizi ya pombe hizo, Serikali itatumia Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 ambapo alitumia fursa hiyo kutangaza utaratibu
wa utekelezaji wa maamuzi hayo.
Alizitaja taratibu hizo kuwa ni
pamoja na kutungwa kwa kanuni zitakazodhibiti uzalishaji wa vifungashio
vya plastiki kwa mujibu wa kifungu 230 (2) (F) CHA Sheria ya mazingira
ya 2004.
Aidha Waziri Makamba ametoa wito
kwa wazalishaji wa pombe kali wanaohitaji muda wa ziada wa kuhamia
katika teknolojia ya chupa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya kupewa
kibali cha kuendelea na uzalishaji huku wakihama kabla ya tarehe 28
Februari.
Makamba alisema kuwa maombi hayo
yaambatanishwe pamoja na ushahidi wa barua ikionyesha mwenendo wa
ulipaji wa kodi, nyaraka kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kuhusu
usalama wa kinywaji, uthibitisho wa Shirika la Viwango
Tanzania(TBS),cheti cha tathmini ya athari za mazingira, uthibitisho
kuwa atatumia teknolojia ya kudhibiti utengenezaji wa vifungashio bandia
na uthibitisho kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni.
Katika hatua nyingine Waziri
Makamba amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini kuendesha operesheni kwa ajili
ya kudhibiti uingizwaji wa pombe kali zinazotoka nje na kuzuia matumizi
ya pombe haramu aina ya Gongo.
Utekelezaji wa uamuzi huo
unafuatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kusitisha matumizi ya
vifungashio vya plastiki ikiwemo pombe za viroba iliyotolewa bunge mwezi
Mei 2016, Agosti na Desemba 2016 na kufuatiwa na agizo la Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa ziarani mkoani Manyara aliagiza
kusitishwa kwa utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zunazofungashwa
kwenye vifungashio vya plastiki kuanzia tarehe 1 Machi
No comments:
Post a Comment