Wanyeviti katika Manispaa ya Kinondoni wakiwemo venyeviti wa mitaa wametakiwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za vyama vyao.
Akito wito huo mkuu wa wilaya hiyo ALI HAPI wakati akizungumza na watendaji wa kata ya Ndugumbi amesema baadhi ya watendaji hasa wenyeviti wa mitaa ktk baadhi ya sehemu wamekuwa wakilalamikiwa kwamba wanabagua wananchi kwa itikadi za vyama vyao hali inayochangia pia kukosa huduma muhimu za kijamii.
Ametolea mfano upo mtaa mmoja ukionekana chama fulani hupati maji kwasababu kiongozi wa mtaa huo anatoka chama fulani na chama kingine huruhusiwi kuchota maji.
Ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha hivyo siasa na vyama vya siasa visiwagawe kwani hivyo husaidia ktk kuzipata nafasi hizo za uongozi tu.
Mkuu wa wilaya pia amekagua mradi wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Mwalimu Nyerere huku akimuagiza injinia wa manispaa hiyo SIMON LIACHEMA kuangalia mfumo wa kisasa katika utengenezaji wa matundu hayo ya vyoo ili kuwapa urahisi wanafunzi pindi wanapotumia vyoo hivyo.
No comments:
Post a Comment