• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 25 February 2017

    Hapi atangaza vita na wavamizi maeneo ya wazi kata ya Wazo

    Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewahakikishia wananchi wa kata ya Wazo kutatua matatizo ya ardhi ambayo ndio tatizo kubwa katika kata hiyo.
    Aidha ametambua maeneo ya Nakaletwa, Chasimba pamoja na viwanja vya mafuriko mtaa wa Kisanga, atashirikiana vizuri na wahusika ili tatizo hilo liishe na muafaka upatikane.
    Hapi amesema watapima maeneo yote ya mashamba yanayomilikiwa na watubinafsi na Manispaa watayapima kwa lengo la kuwasaidia wananchi. Wakisha yapima watapata vibali na watafanyia mambo mengine ya maendeleo. Faida moja wapo ya upimaji wa maeneo hayo kuwa matapeli hawatojitokeza kwani kila mmoja atakuwa na vibali.
    Amewaomba watendaji wa Wazo, Bunju, Tegeta ma Mabwepande kukaa pamoja na kuchagua eneo la dampo ili wakazi wa eneo hilo wapate unafuu na magari ya kubebea takataka yatapunguza kutembea umbali kidogo.  Huku akiwapa salamu wavazi wa maeneo ya wazi wa kata hiyo kuwa atawashughulikia ipasavyo kwa mujibu wa sheria.
    Aidha Kwa taarifa ya mtendaji wa kata hiyo amesema kata ina shule 7 za serikali zikiwa 3 na binafsi 4, huku kukiwa na barabara za rami 4 kata nzima naye akiongeza kuwa mgogoro mkubwa ukiwa ni Ardhi pamoja na changamoto mbalimbali.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI