• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday 25 February 2017

    Sam wa Ukweli avunja ukimya


    Staa wa Bongo Flava Sam wa Ukweli, anapania kuachia kibao kipya hivi karibuni. Sam ambaye amekuwa kimya kwa muda sasa anahisi ni wakati muafaka wa yeye kuikata kiu ya muziki kwa mashabiki wake.
    Hata hivyo kibao hiki kwa jina Nawaona kinatarajiwa kuwa kibao kinachoeleza ugumu uliopo kwenye game ya muziki wa Bongo Flava kwa sasa. Hit maker huyo wa ‘Hata Kwetu Wapo’ alimtumia sample ya nyimbo hiyo mkali wa Muziki Majanga Dogo Rich ambaye walishawahi kufanya collabo pamoja awali ilikuisikiliza.
    Dogo Rich hakusita kueleza ujumbe uliopo katika kibao hiki Nawaona kwani ujumbe uliopo kwenye ngoma hii unaonekana kushabihiana na ujumbe wa Muziki Majanga. Rich alitumia ukurasa wake wa Facebook kumwaga mtamaa kwenye kuku wengi kwa maneno haya yafuatayo.
    Ndugu yangu Sam kanitumia nyimbo karibu inilize…yaani usidhani majanga yapo kwetu…wenzetu pia wanayapitiw japo wako kimya.. richie nimetoa hits kibao tu ..Naonaraha..sinaraha hayanamjuzi…yoyobah na baadae majanga eti natafta kiki …kwani nilikua cjulikani daaaa tafuta nyimbo ya sam itakugusa sana….
    Kunani? Maneno haya yanavutia na yamewatia mashabiki wengi hamu ya kujua kibao Nawaona kimebeba nini. Je Sam Wa Ukweli atatumia fursa hiyo kuwataja mastaa wakubwa Bongo na maisha yao wakiwemo ma producer na waimbaji kama alivyofanya Richie ama bahasha hii mpya imebeba kitu gani ndani yake? Sisi letu jicho na masikio tayari tumeyafungua kuona na nini Sam Wa Ukeli anatuletea.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI