Sakata la dawa za kulevya limezidi kuchukuwa sura mpya ncini baada ya jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutangaza list ya baadhi ya mastaa akiwemo TID, Rachel, Chid Beenz, Babuu wa Kitaa, Rommy Jons, Petit Money, Nyandu Tozzy, Mr Blue na askari polisi wasiopungua 9 kuwa wanatuhumiwa kuhusika na mtandao wa dawa za kulevya aidha kwa kutumia au kufanya biashara, na kuwataka wahudhurie kituo cha polisi cha kati ‘Central Police’ kwa mahojiano ambapo baadhi yao walitii wito huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kueleza kinachoendelea kwenye oparesheni ya kuuibua mtandao wa watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya RC Makonda ameeleza kuwa wamefanikiwa kuwabaini askari watatu wanaofahamika kwa majina ya Nuh Zungu, Fadhili na Ben ambao walikuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya na taarifa iliyopo wamepewa takribani bilioni 1 na wafanyabiashara wa dawa za kulenya.
Pia RC Makonda amewataja watu wengine watano wanaotuhumiwa akiwemo Omary Sanga ambaye anadaiwa kuhusika kusafirisha watu mbalimbali kuelekea nchini China kwa biashara hiyo na zaidi ya watanzania kwa 65% waliokamatwa nchini humo wamepelekwa na yeye, hivyo amehaidi kuwa vyombo vya usalama vitamshughulikia, wengine aliowataja ni Kashozi, Amani, Alidar,Kavila.

Huku kwa upande wa wasanii akiwataja msanii mahiri wakike hapa nchini Vanesa Mdee na mlimbwende wa kwenye video mbalimbali za wasanii maarufu kama Tunda, na kuwataka wafike siku ya Jumatatu saa mbili asubuhi katika kituo hicha cha kati, na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watawasaidia kujua wapi wanazipata hizo dawa na kama wana sambaza wanawasambazia kinanani ili mtandao wote uweze kujulikana, na kuwataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwani vita hii siyo ya Makonda, Sirro wala Rais Magufuli alieleza RC Makonda.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamanda Sirro ameeleza kuwa waliofika leo kwa upande watu mashuhuri na kawaida ni 5, huku polisi wakiwa ni 10 na kufafanua kuwa wawili wapo uhamishoni hivyo watatuma taarifa kwenye mamlaka husika ili waweze kuletwa kwa mahojiano zaidi, huku akieleza kuwa kufuatia suala hilo wameunda TASK FORCE inayoundwa na vyombo vyote vya usalama kwa ajili ya suala hilo la mtandao wa dawa za kulevya inayoongozwa na RC Makonda.

No comments:
Post a Comment