ahmed
Serikali ya kanada imeahidi kutoa shilingi billion sitini kwa ajili ya kusaidia za Wazalishaji wadogo wadogo ili waweze kujipanua na kukuza biashara zao.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na uwekezaji Dk. Adelheim Meru Kwenye uzinduzi wa progamu ya kuza biashara sawia ambayo imelenga kuendeleza viwanda vidogovidogo ambapo amesema kuwa fedha hizo zitatolewa bure kwa lengo la kuhakikisha wafanya biashara hao wanashiriki kikamilifu katika kukuza sekta ya viwanda na kuinua uchumi wa nchi.

Aidha amebainisha kuwa lengo kuu la mradi ambao ni ufadhili wa Serikali ya kanana kupitia taasisi ya meda Tanzania umeanza kwenye mikoa mitano ukiwenmo mkoa wa Mtwara, Arusha, Morogoro na Dar es Salaam ni kuwaongezea mitaji wajasiriamali pamoja na kuwapa teknolojia mpya ufundi na ujuzi ili waweze kuzalisha kwa wingi.
“Program hii inaendana na Sera ya nchi ya sasa kwani tunahitaji Tanzania ya Viwanda hivyo basi, kwa miaka hii sita tunategemea tutakuwa tumeshaongeza wazalishaji zaidi ya elfu kumi”. Alisema Dk. Meru
Naye Mwakilishi kutoka Chama cha wanawake Tanzania Dina Bina amesema kuwa Meda itawasaidia kukuza biashara itakayolenga kukuza mnyororo wao kama wajasiriamali wanawake nchini kwani kupitia mradi huo watafahamu wapi Bidhaa ipi itauzika kwa wingi,


No comments:
Post a Comment