Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea
amesema tangu Chadema ichukue halmashauri mbalimbali jijini hapa
imefanikiwa kuokoa Sh 1.2 bilioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho ya
madiwani Kinondoni na Ubungo kwa mwaka.
Kubenea ameyasema hayo leo wakati
alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya
kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.
“Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni
zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800
milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka
upele,” amesema Kubenea.
Kubenea amefanya ziara hiyo na itakuwa muendelezo wa kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo la Ubungo
No comments:
Post a Comment