BAADA ya kupata dhamana ya Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf
Manji, amelazwa tena kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
iliyoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa
na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo jana, Anna Nkinda, Manji alifikishwa
hospitalini hapo juzi jioni ikiwa ni muda mfupi baada ya kupata dhamana
dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili.
“Ni kweli Manji yupo hapa, aliletwa jana
jioni (juzi) kwa matibabu ambapo hadi leo (jana) ninavyoongea na wewe
bado yupo hapa amelazwa anaendelea na matibabu kama kawaida,” alisema
Anna.
Hii ni mara ya pili kwa Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kulazwa kwenye taasisi hiyo.
Mara ya kwanza ilikuwa ni Februari 12,
mwaka huu alipolazwa hapo akitokea katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es
Salaam, alipokuwa ameshikiliwa tangu Februari tisa akifanyiwa mahojiano.
Mfanyabiashara huyo alifika mwenyewe
kwenye kituo hicho cha polisi kutokana na wito uliotolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaja majina 65 ya watu aliodai
wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mbali na Manji, baadhi ya watu wengine
waliotajwa na Makonda na kutakiwa kufika kituoni hapo ni Mchungaji wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mbunge wa zamani wa
Kinondoni, Idd Azzan ambao tayari wamehojiwa polisi huku Mbunge wa Hai,
Freeman Mbowe, akiwa bado hajahojiwa licha ya kutajwa kwenye orodha
hiyo.
Juzi Alhamisi, Manji alifikishwa kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo shauri lake lilisikilizwa na
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha.
Karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi,
alimsomea mshtakiwa shtaka lake ambapo alidai kuwa kati ya Februari 6 na
9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View jijini Dar es Salaam, Manji
alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo na
Mkurugenzi wa Mashtaka Msaidizi (ADPP), Osward Tibabyekomya, alidai kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga
tarehe nyingine ya kutajwa.
Upande wa mawakili wa utetezi ambao ni
Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, waliiomba Mahakama kumpa mshtakiwa
dhamana kwa sababu ya mashtaka yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Mkeha alisema mshtakiwa atakuwa
nje kwa dhamana kwa kutakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10
pamoja na mdhamini mmoja wa kuaminika ambapo Katibu Mkuu wa Klabu ya
Yanga, Charles Mkwasa, alimdhamini Manji, ambaye aliachiwa kwa dhamana
hadi Machi 16.
Mara baada ya kupata dhamana, Manji aliondoka mahakamani hapo saa 9:40 akiwa kwenye gari yenye namba T670 BBX aina ya Humme
No comments:
Post a Comment