MEYA wa jiji
la Dar es Salaam Isaya Mwita ,amewataka wazazi wa jijini hapa kuhakikisha
kwamba wanashirikiana kikamilifu na bodi za shule ili kuleta mabadiliko ya
matokeo ya wanafunzi wanao maliza masomo yao.
Aidha amewataka
wazazi kuwaweka watoto wao kwenye misingi mizuri ya kimaadili ikiwemo kutumia
mitandao, simu za mkononi kwakuwa nijambo linalofanya watoto kufanya vibaya
kwenye mitihani yao.
Meya Isaya
alitoa kauli hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki aliposhiriki ibada na waumini
wakanisa la Ufufuo lililopo Kimara Bonyokwa jijini hapa ambapo pamoja na mambo
mengine alisema kwamba suala la matokeo mabovu yaliyopatikana katika jiji
linaweza kuhusisha na mambo ya mitandano kutokana na kwamba watoto wengi
sikuhizi wanatumia muda mwingi kwenye mitandao badala masomo.
Alisema suala
la mitandao kwakisi kikubwa kimefanya jiji la Dar es Salaam kupata matokeo hayo, kwakuwa wazazi wameruhusu watoto
wao kutumia simu ambazo zinajihusisha na mambo ya mitandao.
“ Hivi sasa
kila mwanafunzi anatumia simu za smati ambazo zinamitandao ya Watasp,
Istragram, Tango, Facebook, na mambo mengine , sasa muda mwingi sana wanaingia
kwenye mitandao kwa ajili ajili ya kuwasiliana kwa njia ya mitandao badala ya
kusoma, na wazazi wanawaangalia , nawao ndio wanawanunulia hizo simu, kwakweli
jambo hilo kama wazazi hawatabadilika inadidi iwekwe sheria ya kudhibiti jambo
hilo” alisema Meya Isaya.
Alisema kwamba
walimu shuleni wasihofie kuwakemea watoto, kuwanyang’anya simu wanafunzi pindi
wanapowaona wanatakiwa kuweka mkazi kwa
wanafunzi ambao wanatumiasimu za mko
Aliongeza kwamba
, kila mzazi anatakiwa kushirikiana na bodi za shule,kwa kila eneo waliopo ili
kushirikiana kikamilifu katika kuweka mipango endelevu ya kuwasaidia watoto katika
suala zima la elimu badala ya kusubiri serikali kufanya kila jambo.
Alisema kuwepo
kwa sera ya elimu bure isifanye wazazi washindwe kujihusisha kwenye michango ya
kupeleka maendeeo badala yake wanatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye maeneo
ambayo wanahitajika.
“ Tuna sera
yetu ya elimu ambayo ni ya elimu bure, jambo hili lisifanye wazazi kutumia
serikali kila kitu, lazima tuige mifano kutoka kwa wenzetu wa Kenya, Uganda
ukienda utaona wanavyoshirikiana na serikali vizuri, bila kujali kwamba jambo
hili linatakiwa kufanywa na serikali” aliongeza.
No comments:
Post a Comment