Ofisi ya Taifa ya Takwimu
imepokea msaada wa pikipiki 14 zenye thamani ya shilingi milioni 66
kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukusanyaji takwimu sahihi kwenye
baadhi ya mikoa
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia
Bi.Nadia Belhaji Hassine alisema lengo la kukabidhi msaada huo ni
kuboresha kazi ya ukusanyaji takwimu mikoani hasa sehemu ambazo
hazifikiwi kwa usafiri wa gari.
Bi. Hassine amesema kutokana na
kazi inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha
ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na
matokeo chanya taasisi hiyo imeamua kutoa msaada huo ili kuimarisha
utendaji wa taasisi hiyo uweze kuwa bora zaidi.
Akizungumza kwenye hafla ya
makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema msaada huo utaboresha na kukuza
tasnia ya takwimu ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
Dkt Chuwa alisema msaada huo
utarahisiha usafiri wa kutoka eneo moja la utafiti hadi lingine na
kuweza kusaidia katika upatikanaji wa taarifa muhimu za kitafiti.
Akipokea moja ya pikipiki hizo
Bw.Lugome Kalisto kutoka Ofisi ya Takwimu Mkoa wa Pwani aliishukuru
Benki ya Dunia kwa msaada wa pikipiki hizo kwani wamekuwa wakipata shida
ya usafiri katika ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo usafiri wa
gari haufiki.
”Tumekuwa tukipata shida katika
ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kwa gari
hali ambayo imekuwa ikifanya utendaji wetu kuwa duni.Alisema Bw.
Kalisto.
No comments:
Post a Comment