Mhe. Mabula akikagua mifumo ya
ulipaji kodi ya pango la Ardhi sambamba na kuhakiki kumbukumbu za
umiliki wa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Ikiwa Operesheni Lipa Kodi ya
Pango la Ardhi inaendelea, ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi inaendelea kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya
pango la Ardhi huku ikiendelea na kuhabarisha Umma kuhusu umuhimu wa
kuzingatia Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, katika vifungu Na. 49 na
51 ambavyo vinadhihirisha ruhusa ya mmiliki kufutiwa umiliki wa ardhi
kama mmiliki hatazingatia kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
Kwa upande wake; Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb), amekuwa
akifanya ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi
sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment