Watoto wa Baraza la watoto Shehia
ya Kiembesamaki wakionyesha igizo lenye maudhui ya udhalilishaji watoto
wakati wa sherehe za kulizindua baraza hilo.
Katibu wa Baraza la Watoto Shehia
ya Kiembesamaki Zulfa Mohd Masanja akisoma risala wakati wa sherehe za
ufunguzi wa Baraza hilo zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki, Wilaya
ya Magharibi ‘B’.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa
Baraza hilo, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae pia ni Waziri wa
Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia maonyesho ya watoto wa Baraza hilo
(kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya watoto Zanzibar Mundhir
Hamdan Said.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto
Shehia ya Kiembesamaki Bimkubwa Haji Hassan akimkaribisha mgeni rasmi
kuzindua Baraza la watoto la shehia hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la
Kiembesamaki ambae ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizindua
Baraza la Watoto wa Shehia ya Kiembesamaki katika sherehe zilizofanyika
Tawi la CCM Kiembesamaki.
Baadhi ya watoto wa Shehia ya
Kiembesamaki wakimsikiliza Mwakilishi wao Mahmoud Thabit Kombo wakati
wa uzinduzi wa Baraza lao kwenye sherehe zilizofanyika Tawi la CCM
Kiembesamaki Wilaya Magharibi ‘B’.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar
No comments:
Post a Comment