JAJI Mkuu anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na
majaji ambao wanadaiwa kuvuruga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha
na dawa za kulevya.
Hayo
ameyasema leo Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini
Rogers Sianga wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na
waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema
kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote
watakaobainika kuhusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo
wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema
kuwa watazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili
kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu
zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.
Nae
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya
majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto
umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Amesema
kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha kufanya biashara ya madawa ya
kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni,ambayo
mojawapo wanatarajia kuifanya usiku wa leo.
Nae
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed almaarufu kwa jina la
kisanii TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana na
watu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya
kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.

No comments:
Post a Comment