• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 17 February 2017

    RC Makonda Akifungua Mkutano wa kujadili mikakati na njia sahihi za kuutokomeza ugonjwa wa kipindupindu

     Akifungua Mkutano wa kujadili mikakati na njia sahihi za kuutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka watumishi wa idara za afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali ikiwemo kuvitumia vyombo vya habari ili ugonjwa huo usiendelee kupoteza maisha ya watanzania wengi.
    RC Makonda ameeleza kuwa tangia ugonjwa huo uliporipotiwa kwa mara ya kwanza 15 Agosti 2015 idadi ya waathirika imeongezeka na kufikia 5180 huku watu 80 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, hivyo elimu na uhamasishaji unahitajika ili watu wengi wasiweze kupoteza maisha.
    Nakusisitiza kuwa kampeni ya usafi iwe endelevu kwani usafi unaanzia nyumbani, na kuwataka watanzania wasiwe na kasumba ya kuona kuwa wakifanya usafi yeye ndiye anapata sifa kwani suala hilo linatija kwa watu wote, na kuwataka watumishi hao licha ya elimu waje na mikakati ya kutokomeza kabisa ugonjwa huo.
    Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Afya ameitaja Dar es Salaam kuongoza kitaifa kwa kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo kuna waathirika 5098 huku vifo vikiwa 47, kiwilaya kwa mkoa huo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha Kinondoni inaongoza kwa kuwa na wagonjwa 2337 vifo vikiwa 18, Ilala 1804 waathirika na vifo 4, huku Temeke ikiwa na waathirika 955 na vifo 16, na kupendekeza changamoto za maji safi na salama zishughulikiwe, uuzwaji holela wa chakula, uwepo wa taka ngumu.
    Pia muwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Grace Sabuti amesisitiza kuwa uwepo wa takwimu sahihi za ugonjwa wa kipindupindu utasaidia kuleta suluhisho  hivyo ni vyema mamlaka husika ikalisimamia hilo ipasavyo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI