• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 1 February 2017

    TGNP umeanzisha semina ya siku tatu Kwa lengo la kutathmini mafanikio

    Image result for tgnp tanzaniaNa Ahmed Kombo
    Mtandao wa kijinsia Nchini (TGNP) umeanzisha semina ya siku tatu Kwa lengo la kutathmini mafanikio yao pamoja na kumkombao mwanamke kuepukana na adha ya maji.

    Mkurugenzi mtendaji wa mtandao huo Lilian Liundi amesema semina hiyo imeanza  mapema hii leo jijini Dar es salaam na inatarajiwa Kumalizika februari 3 mwaka huu ambapo amesema wanatathmini ni kwa kiasi gani wamefanikiwa kupunguza adha ya maji Nchini.

    Hata hivyo mwanachama muanzilishi wa mtandao huo Asseny Muro amesema wameshafanikisha kwa kiasi fulani katika kupunguza adha ya maji vijijini na mijini.

    Muro amesema Mwanamke amekuwa akitumika katika shughuli za kuchota maji majumbani kuliko kufanya mambo mengine ya kimsingi hivyo semina hiyo itaangazia pia ni kwa namna gani wanamkomboa mwanamke na adha hiyo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI