Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venanche Mabeyo akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia Madawa ya Kulevya Nchini Rogers William Sianga wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul
Makonda wakizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la
Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye, Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya NdaniMhe Mwigulu
Nchemba wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi wa kikao
cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia Madawa ya Kulevya
Nchini Rogers William Sianga akijitambulisha mbele ya Baraza la Taifa
la kudhibiti Dawa za Kulevya wakati Waziri Mkuu alipokuwa akizindua
Baraza Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
akizungumza na Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Udhibiti wa
Dawa za Kulevya Nchini wakati akifungua kikao cha Baraza hilo leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la
kudhibiti Dawa za Kulevya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la
kudhibiti Dawa za Kulevya.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
…………………………………………………………………………….
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa hatua kali
zitachukuliwa kwa atakayepokea rushwa kutoka kwa wauzaji, wasambazaji na
watumiaji wa Madawa ya Kulevya.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es
salaam wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Taifa la
kudhibiti dawa za kulevya nchini.
“Sheria ya udhibiti wa madawa ya
kulevya itumike vizuri, Serikali na Baraza halitahitaji mtu yeyote
mwenye mamlaka kupokea rushwa ikigundulika hatua kali zitachukuliwa”
alifafanua Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kuimarisha mapambano
dhidi ya udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini ambayo yamekuwa yakifanywa
na Serikali za Awamu zilizotangulia.
Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa
mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ni vita inayotakiwa kupigana kwa
nguvu kubwa kwani madhara ya dawa hizo ni kubwa kwa jamii hususani
vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.
“Tunahitaji ushirikiano wa karibu
wa pande zote mbili za Muungano kwani tatizo hili limeathiri pande zote
na ukanda wa bahari unatumika sana kama njia ya kuingiza dawa hizo”
“Wakuu wa Mikoa mna kazi kubwa
katika vita hii, mkiwa wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama mpo
kwenye nafasi nzuri ya kuendesha vita hii kwa mujibu wa Sheria, Kanuni
na Taratibu zilizopo” alisema Waziri Mkuu.
Hata hivyo Waziri Mkuu
alibainisha kuwa, wajibu wa Baraza ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya
Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, ambapo jukumu hilo ni kubwa na
wajumbe wa Baraza hilo wanatakiwa kulitekeleza kwa uadilifu na umahiri
mkubwa.
Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa
za Kulevya limeanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Kudhibiti
na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 ambapo Waziri Mkuu
ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo pamoja na wajumbe wengine wakiwemo
Waziri anayeshughulikia Mambo ya Sheria, Waziri anayeshughulikia Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Wengine ni Waziri
anayeshughulikia Afya, waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii,
Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nchi za Nje, Waziri anayeshughulikia
Fedha, Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Waziri
anayeshughulikia Elimu, Waziri anayeshughulikia Kilimo, Waziri
anayeshughulikia Uchukuzi na Waziri anayeshughulikia Ulinzi
No comments:
Post a Comment