Dk. Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ametoa taarifa ya mafanikio ya hospitali hiyo kwa kipindi cha miezi 4 iliyopita huku wauguzi wengi wakipatiwa ujuzi nje ya nchi.
Moja ya mfanikio aliyoyataja ni pamoja na wakunga wa dharura kuongezeka lengo likiwa ni kusaidia kutibu wagonjwa wanaofika katika hispitali hiyo huku kukiwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji tiba kutoka 200 hadi kufikia 300.

Licha ya wakunga bado Muhimbili inasimamia mitambo kwa njia ya mtandao yaani ‘TV’ kwa hospitali 7 ikiwemo Hospitali ya Temeke, endapo watapata wagonjwa katika hospitali hizo huwasiliana moja kwa moja na Muhimbili.
Hospitali pia imewapeleka wauguzi 20 kwa ajili ya kupata mafunzo ya figo na watakaa kwa miezi mitatu kisha wakirudi wanaweza kusaidia wagonjwa ambao wangesafiri hadi India iliwa kuokoa pesa za serikali kwani kwa mgonjwa mmoja inagharimu milioni 80 kumsafirisha; huku kukiwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa 95% na wako katika mpango wa kuongeza majengo ya upasuaji.
Akigusia suala la madawa ya kulevya Dk. Swai amesema uhitaji wa dawa za Methadone umeongezeka hii inatokana na wagonjwa kuwa wengi, licha ya mafanikio bado kuna changamoto ya rasilimali watu, uchakavu wa miundombinu pamoja na msongamano wa watu
No comments:
Post a Comment