Imeelezwa kuwa uchafuzi wa Mazingira utokanao na Zebaki huigharimu Tanzania kiasi cha Shilingi Billioni 7 mpaka 9.5 kila mwaka kama ilivyoainishwa na utafiti Mpya katika Jarida la Usimamizi wa Mazingira.

Taarifa hiyo iliyofanyiwa mapitio na wataalamu wa Sayansi kutathmini athari za kiuchumi zitokanazo na kuharibika au kupungua kwa uwezo kiakili (IQ) utokanao na uchafuzi wa Zebaki Tanzania pamoja na Nchi nyingine 14 Duniani.

Akizungumza na wanahabari wakati wa uwasilishaji wa Matokeo hayo ya utafiti huo Afisa Miradi Mwandamizi kutoka Asasi ya kiraia inayojishughulisha na Masuala ya Kemikali na taka hatarishi (AGENDA) Haji Rehani amesema kuwa utafiti huo ulionesha asilimia 64 ya wale waliochukuliwa sampuli za nywele katika utafiti huo walikuwa na kiwango cha juu hasa wale wanaoishi maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini.
“Zebaki hutumika katika maeneo hayo ili kukamatisha Dhahabu na kuchomwa ili kupata Dhahabu, huku taka hizo pamoja na maji yatumikayo katika mchakato huo hutiririka na hatimaye kuingia katika Mito ya jirani ambayo hutumiwa na Jamii”. Alisema Rehani
Aidha Rehani amebainisha kuwa utafiti huo ulionesha pia kiasi kidogo cha athari ambayo inatokea pia sehemu nyingine zenye shughuli zionazofanana na maeneo hayo nchini hivyo basi kuna uhitaji wa kuridhia na kuutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki ili kuzuia Upotevu unaoweza kutokea kutokana na Uchafuzi wa Mazingira Nchini.


No comments:
Post a Comment