Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na Maafisa na Askari wa vyombo
vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake, katika Ukumbi wa
Bwalo la Magereza, mjini Kilwa mkoani Lindi. Masauni aliwataka maafisa
na askari hao kuongeza nguvu zaidi katika ukamataji wa wahamiajiharamu
pamoja na wauza dawa za kulevya.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Lindi, Renatha Mzinga (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa
anakagua Makazi ya askari Polisi, Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za
askari hao zimechangaa na chache kutokana na wingi wa askari hao. Hata
hivyo, Serikali hivi karibuni inatarajia kujenga nyumba mpya katika eneo
hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,
Renatha Mzinga akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni eneola Mitwero mkoani humo ambalo nyumba za
makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni alikagua nyumba
wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo hilo makazi mapya
yatakapojengwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akilikagua Jengo jipya la
ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi ambalo linajengwa mjini humo.
Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George Kombe, pamoja na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga. Masauni aliongozana na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo
kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (wapili kushoto), wakati Naibu Waziri
huyo alipokuwa anaangalia ramani ya ujenzi wa makazi ya askari polisi
eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara
ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey
Zambi (kulia) akimkaribishaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni ofisini kwake kwa ajili ya kupewa taarifa ya mkoa
huo, wakati Naibu Waziri Masauni alipofanya ziara ya kikazi mkoani
humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment