Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano
wa mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,
uliofanyika Jijini Mwanza.
Judith Ferdinand, BMG
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.
Elimu
hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa mashauriano kati ya
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la
Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka, uliofanyika katika ukumbi wa Rock
City Mall Jijini Mwanza.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene
Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili
kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka
2010 bila vikwazo pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za
bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za
ujenzi.
Dkt.
Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa
Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa
msaada wa haraka pale unapohitajika.
Pia
amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442 lakini wamaotenda kazi ni
wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la
Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza kama
umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao
vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.
Kwa
upande wake Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye
ndiye mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na
Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki
kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka
2010.
Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina wataalamu wake.
“Ikumbukwe
kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa
taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi
kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi,” alisema Marijani.
Naye
DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi,
hivyo kujua chanzo cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka
kwa wahandisi.
Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment