• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 6 March 2017

    MWANASHERIA TUNDU LISSU AKAMATWA NA JESHI LA POLISI

    Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu anaripotiwa kukamatwa na Polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar huku sababu za kukamatwa zikiwa bado hazijajulikana.
    Taarifa ambayo imetolewa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene imesema kuwa Tundu Lissu amekamatwa wakati akitoka Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili ya uchochezi.
    “Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi muda mfupi uliopita na anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) jijini Dar es Salaam. Hadi sasa polisi hawajasema sababu ya kumkamata na kumshikilia Tundu punde tu baada ya kutoka Mahakama ya Kisutu ambako kesi dhidi yake kuhusu tuhuma za uchochezi ilikuwa imefutwa na mahakama hiyo.” imesema sehemu ya taarifa ya Makene.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI