Rais wa Marekani, Donald Trump ameiondoa nchi ya Iraq katika listi ya nchi ambazo atazuia wahamiaji na wakimbizi kutoka hizo nchi kuingia Marekani, Shirika la Habari la Associated Press limeripoti.
Bila kutaja chanzo cha habari hiyo, AP limeripoti kuwa sababu ya Trump kuiondoa Iraq ni kuifanya nchi hiyo kama moja ya nchi ambazo zinaongoza mapambano dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Islamic State.
Hatua ya Trump kuiondoa Iraq imekuja baada ya mahakama kuondoa agizo alilolitoa la kuzuia wahamiaji na wakimbizi kutoka nchi saba ambazo zina imani kali za Kiislamu ambazo ni Iran, Iraq, Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen.
Agizo mpya la Trump kuzuia wahamiaji na wakimbizi kuingia Marekani linatarajiwa kutolewa jumatano ya Machi mosi.
No comments:
Post a Comment