Michezo
Robo
Fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation
Cup 2016/2017), kati ya Azam FC na Ndanda FC itafanyika kesho Aprili 5,
2017 saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam, imefahamika.
Kadhalika,
Robo Fainali ya nne ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam
Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania
Prisons FC itafanyika Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam.
Tayari timu za Mbao FC ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam, zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali.
Mbao
iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa
Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, 2017 ilihali Machi 19, mwaka huu Simba
iliilaza Madini ya Arusha kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid jijini Arusha.
Bingwa
wa michuano hi ambayo msimu huu ilishirikisha timu 86 ikiwa ni pamoja
na za Ligi Kuu ya Vodacom (timu 16); Ligi Daraja la Kwanza (timu 24);
Ligi Daraja la Pili (timu 24) na mabingwa wa mikoa timu 22, atawakilisha
nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho – CAF.
No comments:
Post a Comment