Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa uongozi wa
Kampuni ya ujenzi ya Chicco, wakati alipokuwa akikagua barabara ya
Kia-Mererani yenye urefu wa KM 26, mkoani Arusha, leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikaza nati katika daraja la
Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 wakati alipokagua barabara hiyo,
mkoani Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akikagua moja
ya daraja lililopo katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM
14.1 inayojengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hanil Jiangsu J/V
wakati alipokagua barabara hiyo, mkoani Arusha leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa eneo la
Sakina mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina-Tengeru
yenye urefu wa KM 14.1.
…………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya mchepuo (Arusha
bypass) yenye urefu wa KM 42.4 na kumtaka mkandarasi M/S Hanil Jiangsu
J/V anayezijenga kuhakikisha zinakamilika kwa wakati.
Barabara hizo ambazo zinajengwa
kwa gharama ya shilingi Bilioni 139.34 zina lengo la kupunguza
msongamano wa magari katikati ya jiji la Arusha kwa kuwezesha magari
makubwa kupita nje ya mji.
Aidha, Profesa Mbarawa amewataka
wanachi wa mko wa Arusha kulinda miundombinu yote ya barabara hizo ili
zidumu kwa muda mrefu na kuleta tija inayokusudiwa.
“Tunatumia pesa nyingi sana
kujenga barabara hizi, hivyo nawaomba wananchi tuzilinde na tuzitunze
ili zidumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Profesa. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewapongeza
wajenzi na wasimamizi wa barabara hizo kwa hatua iliyofikiwa na kuwataka
kuongeza kasi ya ujenzi na kuzingatia thamani ya fedha katika barabara
hizo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa
Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Eng. Mgeni Mwanga,
amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara mkoani
Arusha utakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Tumejipanga kuhakikisha barabara
ya Sakina-Tengeru na ile ya mchepuo kukamilika kama ilivyopangwa ili
kupunguza msongamano hali itakayovutia ongezeko la watalii na hivyo
kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha”, amesema Eng. Mwanga
No comments:
Post a Comment