• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 26 April 2017

    Dc mjema azindua ujenzi wa barabara pugu


    Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amezindua ujenzi wa barabara ya kutoka Pugu mpaka Majohe kwa kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita saba.
    Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo DC Mjema ameeleza kuwa serikali imeamua kuzindua ujenzi huo ambao utachukua muda wa miezi mitatu mpaka kukamilika kwake, baada ya kupata malalamiko kuwa wananchi wamekuwa wakipata hadha kubwa ya usafiri kwani barabara hiyo imekuwa haipitiki kipindi cha mvua na kupelekea barabara kujaa maji.
    Vilevile kuhusu ujenzi huo DC Mjema ametoa tahadhari kwa wanaoishi kwenye hifadhi ya barabara kubomoa nyumba zao mara moja kabla serikali haijachukua hatua, huku akisisitiza kuwa hakutakuwa na fidia yeyote kwa watakao bomolewa.
    Katika hatua nyingine DC  Mjema ametembelea dampo la Pugu Kinyamwezi na kupokea lawama mbalimbali kutoka kwa wakazi waishio eneo hilo akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Viwege kata ya Majohe Amina Rashidi wakilalamikia miundombinu mibovu ya dampo hilo ambalo limekuwa likitiririsha maji machafu kuelekea kwenye makazi yao.
    Akijibu kero hiyo DC Mjema amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuziba matundu yote yanayotiririsha maji machafu kwenye makazi ya wananchi hao, huku wakisubiri utaratibu kutoka Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC), na kuwataka wawe na subira huku akiwataka wale wanaoishi mabondeni kuhama mara moja na serikali itawapatia maeneo ambayo waoa watagharamia gharama za upimaji.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI