Umoja wa Wanawake Watanzania waishio nchini Ubeljiji, ‘Upendo Women’s Group’ leo wametoa msaada wa vifaa vya kwenye wodi ya wajawazito ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
Akizungumza na wanahabari jana wakati wanakabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Upendo Women’s Group, Theresia Greca alisema kuwa wanajua changamoto wanazokutana nazo wanawake wa Kitanzania katika wodi mbalimbali wanazokwenda kujifungua ikiwemo uhaba wa vifaa na changamoto nyingine nyingi.
“Wajawazito wana changamoto nyingi sana wakati wa kujifungua, vifaa ni vichache, wahudumu wachache na changamoto nyingine nyingi, hivyo kama Upendo tumekuwa tukikusanya misaada kwetu na wadau mbalimba kwa ajili ya kusaidia wodi ya wajawazito ya Mwananyamala.
“Hii ni awamu ya tatu kwa Upendo kutoa vifaa kwenye wodi ya wazazi hapa Mwananyamala, leo tunatoa vifaa vifuatavyo: Fetal dopler 1, Speculum- SIMS 3, Speculum-cusco 3, Drum (medium)2, Mackintosh Troll 2, Penguin Sucker 2, Needle Holder 10, Sponge Forceps 10, Ambulance Stretcher 1, Ambubag Infant 2, Clinical Thermometer 30, NGT size 8, Drip Stand 3.
Vingine ni Vacuum Extractor 1, Bed Powder Coated 2, Double Step Powder Coated 6 Istrument Trolley 1, Ressuciatian Trolley 1 ambapo vifaa vyote vimegharimu T.Sh.s Mil. 10310000/= (Milioni kumi na laki tatu na elfu kumi)”
Umoja huo unaundwa na wanawake 14; akiwemo mwenyewe, Theresia Greca, Begum Razafinjatovo na Upendo Shoo ambao ni Waweka Hazina. Wengine Ni Fausta Mneney, Dora Maiga, Rosi Kadaga, Linda Shayo, Agnes Kayola, Sedda Maiga, Kimwisho Mndolwa, Hadija Juma, Imbori Na Editha.
Aidha Upendo imewataka Watanzania kujenga utaratibu wa kuwasaidia wodi za wazazi nchini na pia wamewashukuru sana wadau ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kufanikisha misaada hii akiwemo Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa, Begum Razafinjatovo, Rosi Kadaga, Chental Ramialimanana,”alisema Greca.
No comments:
Post a Comment