Ikulu, Chamwino,Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 28 Aprili 2017, atapokea
Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma katika
Ukumbi wa Chimwaga Mkoani Dodoma.
Taarifa hiyo itawasilishwa kwa
Mheshimiwa Rais na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Mwezi Oktoba mwaka 2016.
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU,
Chamwino, Dodoma.
27 Aprili, 2017
No comments:
Post a Comment