Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita akiwa akisikilia jambo wakati wa mkutano uliomalizika jana
jijini Mashahad Nchini Iran , pembeni yake kulia mwenye baragashea ni
Meya wa jiji la Acra Mohamed Sowah na wakwanza kushoto ni Meya wa jiji
la Kamapa Elias Lukwag.
Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita wapili kulia akiwa kwenye mkutano jijini Mashad Nchini Iran,
wa kwanza kulia ni Meya wa Damascas Nchi Syria
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa kwenye mkutano jijini Mashad nchini Iran
NA MWANDISHI WETU, Mashahad
MEYA wa Jiji la Dar es salaam
Isaya Mwita amekuwa gumzo katika mkutano uliomalizika jana Jijini
Mashahad Nchini Iran baada ya kusema kwamba Tanzania haina dini ila watu
wake wana dini.
Meya ambaye yupo Nchini Iran kwa
ziara ya kikazi ya siku 10, alijikuta kwenye gumzo hilo wakati
akichangia mada iliyokuwa ikiendelea ndani ya mkutano huo ambao
ulimalizika jana.
Meya alisema kwamba Tanzania ni
Nchi ya amani ambayo haijawahi kuwa na ubaguzi wa rangi, dini wala
kabila na kwamba kila mmoja aliyepo ndani ya nchi hiyo anajivunia kuwa
mtanzania.
Alisema hali hiyo imekuwa ni
tofauti hata katika maeneo mengine kwani yapo mataifa ambayo hadi sasa
yanajadili udini na ukabila , na kushauri kwamba ni vema viongozi wa
kila majiji kujitahidi kutumia nafasi hiyo ili kuondokana na matabaka.
“ Watanzania kuna mambo ambayo
tulijiwekea tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo
ndio msingi mkuu tulionao, hakuna ubaguzi wa dini wala rangi, jambo kama
hili ni maeneo machache sana katika Nchi zetu kuyakuta,hivyo Tanzania
tunajivunia kuwa na utamaduni huu” alisema Meya Mwita.
Alieleza kwamba “ Jumuiya za
kimataifa zimekuwa zikiwatazama waislam wote kama watu ambao si salama
nakushauri kwamba haki za kibinadamu zizingatiwe kwao kwakuwa wote
tunaombwa na Mungu mmoja” alisema Meya Mwita.
Aliongeza kwamba “ wapo watu ambao
wanaitumia dini ya kiisilamu vibaya, nakuchafua watu wengine , lakini
tunatakiwa kutambua kwamba kila wote hapa tumeumbwa na mungu mmoja, sasa
dini zetu zisitufanye tukashindwa kushirikiana na kuzungumza lugha
moja” alisistiza.
Hata hivyo katika hatua nyingine
Meya alisisitiza majiji makubwa ya nchi za kiafrika yajielekeze katika
kutatua changamoto za watu wake.
Aidha Meya ametumia nafasi hiyo
kuwakaribisha Wailan kuja kuwekeza katika Nchi ya Tanzania sambamba
katika kuendeleza fursa za kibiashara.
Hata hivyo mkutano huo umemalizika
na kwamba Meya kesho ataelekea jijini Tairan kwa mualiko wa Meya wa
jiji hilo ambapo pamoja na mambo mengine huko atatembelea ofisi za umma
na kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya kujadili namna ya
kuendesha majiji sambamba na kutatua changamoto.
No comments:
Post a Comment