Msanii mkongwe wa muziki, Ray C, amedai kwa sasa anapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika muziki wake.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma na
wimbo ‘Mapenzi Matamu’, alikuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu
akijaribu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zlimuathiri kwa
kiasi kikubwa.
Akiongea na Bongo5 wiki hii akiwa mwenye siha njema, Ray C amedai
anachokifikiria kwa sasa katika maisha yake ni muziki na siyo mapenzi.
“Mimi sina mpenzi,” alisema Ray C “Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki
wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu
wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao
wanataka kazi, muziki mzuri,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya Wasafi.Com ya Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Unanimaliza’.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya albamu yake mpya.
No comments:
Post a Comment