Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari kwa umma kuhusu
vipindi vya mvua kubwa vinavyoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa
katika mwambao wa ukanda wa pwani.
TMA katika taarifa yake imetoa tahadhari kuwa, kuanzia leo hadi kesho
kutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50
ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa
saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya
Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na
Pemba.
“Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini na
kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika Bahari ya Hindi eneo la
kisiwa cha Madagascar, hivyo kusababisha upepo mkali katika pwani ya
Tanzania,” imesema taarifa hiyo.
TMA imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki.
Soma taarifa kamili:
Na Emmy Mwaipopo
No comments:
Post a Comment