Kabla ya Dunia kusimama kwa muda hii leo kupisha Mpambano wa
kusisimua wa Mchezo wa Masumbwi Duniani, Legendari wa Mchezo huo Mike
Tyson, amejitokeza hii leo na kuweka wazi kuwa Anthony Joshua atashinda
katika pambano hilo.
Joshua ambae ataingia ulingoni kuvaana na Klitschko, anaaminiwa na
Tyson kuidhihirishia Dunia ni namna gani Ngumi za kimarekani zilivyo
katika mpambano.
Legendari Tyson, atakuwa akilifuatilia pambano hilo kwa karibu kabisa
Jumamosi ya leo. mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Wembley na
itakayoshuhudiwa mubashara, Duniani kote kupitia runinga ya Michezo ya
Sky Sport.
Tyson ambaye alikuwa bingwa wa dunia asiepigika katika zama zake, ana matumaini makubwa na Joshua kutwaa ushindi siku ya leo.
No comments:
Post a Comment