Mbali na kupunguza uzito na kuwa kiungo
kizuri sana kinachotumika kwenye vyakula na vinywaji mbali mbali, pia
tangawizi inasaidia kutibu vitu vingi mwilini.
1.Huondoa gesi tumboni:-
Tangawizi
husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi
yanayosababishwa na ulaji. Tangawizi husaidia yote hayo--}
2. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo:-
Wataalamu
wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo
na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia
joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye
ubongo bila shida.
3. Huongeza nguvu za kiume:-
Tangawizi
inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu
katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo.... Dr. Mandai
4.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao :-
Kwa kina mama wajawazito, wanopata kichefuchefu na kutapika inasaidia sana kuondoa hali hiyo.
*Tafuna kipande cha tangawizi, badala ya ndimu. Inasaidia zaidi by Dr. Mandai
*Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi.
7. Husaidia Maumivu ya Viungo:-
Kwa wale wanaosumbuliwa na maumivu ya viungo ya mara kwa mara, chai yenye tangawizi yakutosha kusaidia kupata nafuu.
8.Husaidia maumivu makali kipindi cha hedhi:-
Kwa wale wanawake wanaoteseka na maumivu makali pindi wa wapo kwenye siku zao. Tangawizi yaweza kuwa msaada mkubwa.
*Kama
alivyoshauri Dr. Mandai, ponda tangawizi mbichi, kisha ichemshe kwa
dakika 10, waweza ongeza sukari, au ukainywa kama ilivyo, mara tatu kwa
siku, baada ya chakula. Na ameshauri kuanza siku tatu kabla ya kuingia
kwenye hedhi.
9. Kusaidia kutoa sumu mwilini:-
Pia
tangawizi yaweza kuwa msaada mkubwa sana wakuondoa sumu
zinazosababishwa na ulaji wa vyakula tofauti tofauti. Inauwezo wa
kuondosha mafuta 'CHOLESTEROL' ambayo kujificha kwenye mishipa ya
kupitishia damu na kusababisha magonjwa mengi mwilini ikiwemo ugonjwa wa
moyo. Kama asemavyo Dr. Mandai, waweza kuiandaa kama chai na kuinywa
asubuhi na jioni. Lakini kwa afya bora zaidi, jizoeze kuinywa bila kutia
sukari. Chemsha yenyewe na uinywe kama ilivyo ikiwa na moto wa kiasi,
kama chai.10.Husaidia kupunguza uzito
Kama
tulivyotangulia kusema hapo juu, kuwa tangawizi inauwezo mkubwa sana
wakusaidia mmeng'enyo wa chakula mwilini na kusaidia kuondoa mafuta
mwilini, yale yanayobaki na kusababisha unene.*Ponda tangawizi yako, kisha changanya na maji. Chemsha mpaka utakapo hakikisha kuwa imechemka vizuri, ndipo unywe ikiwa ya moto kiasi, kama chai. Ni vizuri kunywa angalau mara mbili kwa siku. Asubuhi na jioni unapokwenda kulala. Utaona tofauti kubwa. Utaamka mwenye nguvu, bila maumivu yeyote mwilini. Kwa matokeo mazuri na haraka, usiweke sukari, na kipindi cha mchana kunywa maji yakutosha. Lakini kama tujuavyo, tangawizi pekee haiwezi kusaidia kupunguza uzito kama hutaangalia ulacho na kuongeza mazoezi ya aina yoyote yale ili kufanya mwili wako kuwa active. JENGA TABIA YA MAZOEZI, iwe kutembea, kuruka kamba, kukimbia, n.k ili tu, kujiweka FIT Chanzo Mtazamo Halisi Blog




No comments:
Post a Comment