Kaimu Kamishna Kitengo cha
Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay (wa
kwanza kushoto) akizungumza jambo katika mkutano huo uliomalizika leo
Aprili 27,2017.
Washriki wa mkutano huo wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea.
Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c. (katikati) Kateshumbwa akizungumza jambo katika mkutano huo.
Picha zote na Philemon Solomon
Akisoma taarifa hiyo mbele ya
vyombo vya habari Kamishna wa Forodha Nchini Uganda, Dickson c.
Kateshumbwa amesema kuwa mkutano wa Umoja wa Forodha kwa nchi zilizo
kwenye uanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki hufanyika kwa zamu nchi
zote za uanachama. Ambapo kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika hapa
nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa kila mwaka mkutano
huo hufanyika katika ngazi tatu, ambazo ni ngazi zinayohusisha
wataalamu wa masuala ya forodha ambao hutoka katika mamlaka za mapato
za kila nchi wanachama, na ngazi ya pili ni makamishna wote wa forodha
walio katika nchi wanachama huku ngazi ya tatu ni makamishana wote wakuu
ambao jukumu lao huwa ni katika kuidhinisha mipango na mikakati pamoja
na kutoa maelekezo na maagizo kwa ajili ya kuhakikisha mipango na
mikakati inatekelezwa.
Alifafanua kuwa lengo la jumuiya
ya Afrika mashariki ni kuhakikisha inatekeleza miradi mbali mbali ya
forodha yenye lengo la kurahisisha na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara
na wananchi wote wanapata faida kwa ujumla.
Naye Kaimu Kamishna Kitengo cha
Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato hapa Nchini(TRA), Qamdiyay Akonaay
ametaja miradi iliyo katika mfumo huo wa forodha kwamba ni pamoja na
himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za kiforodha, kituo kimoja
cha huduma Mpakani na wafanyabiashara wenye kuidhinishwa huweza kupata
huduma maalumu.
Mkutano huo ulianza Aprili 21
mwaka huu na umemalizika leo Aprili 27 ambapo maazimio mbalimbali juu ya
mkutano huo yamejadiliwa na miongoni mwa hayo ni, mpango wa kuwa na
himaya moja ya forodha, muunganiko wa huduma za kiforodha na mapitio ya
viwango vya ushuru na kanuni za uasili wa bidhaa
No comments:
Post a Comment