Waziri wa habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe
ameiagiza uongozi wa klabu ya soka ya Yanga kupeleka maelezo kwa nini
kikosi cha klabu hiyo hakijafika uwanjani katika sherehe za 53 za
Muungano wa Jamuhuri ya Tanzania, na badala yake kupelekwa kikosi cha
vijana na wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza.
Dr Mwakyembe ameyasema hayo Mkoani Dodoma alipohojiwa na muandishi wa
habari za michezo, sababu za yeye kuondoka mapema katika mchezo huo
kabla kuisha. Baadhi ya viongozi wa soka Mkoani hapo pamoja na wadau wa
soka waitupia lawama klabu hiyo kwa kuwapelekea kikosi chapili badala ya
kile walicho kitarajia.
katika uwanja huo wa Jamuhuri, kumechezwa michezo miwili hapo jana,
ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa ni kati ya Wabunge wa bunge la Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania dhidi ya baraza ka wawakilishi kutoka zanzibar,
mchezo uliomalizika kwa timu ya Bunge la jamuhuri ya muungano wa
Tanzania wakichomoza na ushindi wa magoli 4 kwa 0.
Mchezo uliofuata ulikuwa ni kati ya timu ya kombaini ya majeshi dhidi
ya klabu ya yanga, mchezo uliomalizika kwa kutoshana nguvu ya goli moja
kwa moja.
No comments:
Post a Comment