- WATU WA NNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI WILAYANI SENGEREMA.
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MJUKUU WAKE WILAYANI ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 25.04.2017 MAJIRA YA
SAA 13:40HRS KATIKA MTAA WA NYATUKALA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA
MWANZA, WATU WA NNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA
KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SELFU AMRI
@ MANUNGWA MIAKA 71, ALIYEUAWA KWA KUPIGWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
KICHWANI KWENYE PAJI LA USO NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WATU
WANAODAIWA KUWA NI WANAFAMILIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA
AKIISHI MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE NA SIKU YA TAREHE TAJWA HAPO JUU
BAADHI YA NDUGU WALIKUA WAKIPIGA SIMU YAKE BILA MAFANIKIO, KUTOKANA NA
HALI HIYO NDUGU WALIKWENDA HADI HAPO NYUMBANI KWAKE NA KUKUTA MILANGO
IKIWA IMEFUNGWA LAKINI WALIPOCHUNGULIA DIRISHA LA CHUMBANI KWAKE WALIONA
MWILI WAKE UKIWA UMELALALA KITANDANI NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI.
ASKARI WALIFIKA HADI ENEO LA TUKIO
NA KUFANYA TARATIBU ZA KUINGIA NDANI NA KUUKUTA MWILI WA MAREHEMU
KITANDANI HUKU UKIWA NA JERAHA KWENYE PAJI LA USO, AIDHA BAADA YA
TARATIBU ZA ENEO LA TUKIO KUFANYIKA, ASKARI WALIUCHUKUA MWILI WA
MAREHEMU NA KUUPELEKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA
UCHUNGUZI ZAIDI WA KITAALAMU.
KUTOKANA NA KIFO HICHO ASKARI
WALIFANYA UPELELEZI AMBAPO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WA NNE
WANAODAIWA KUSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA KUFANIKISHA
MAUAJI HAYO, KATI YAO WAPO BAADHI AMBAO WANAMAHUSIANO NA MAREHEMU LAKINI
MAJINA TUNAYAHIFADHI KWA AJILI YA UCHUNGUZI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI
UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, CHANZO CHA
MAUAJI HAYO INADAIWA KUWA NI MGOGORO WA MIRATHI YA MALI ZA FAMILIA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA
WA MWANZA, AKIWAOMBA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KOSA LA JINAI BALI PINDI WANAPOKUWA KATIKA MIGOGORO YA AINA YEYOTE
ILE NA WATU WENGINE WANATAKIWA KUTOA TAARIFA KWA VYOMBO HUSIKA KAMA VILE
POLISI, MAHAKAMA AU MABARAZA YA ARDHI ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE
KUFUATWA NA HAKI IWEZE KUPATIKANA.
KATIKA TUKIO LA PILI,
MNAMO TAREHE 25.04.2017 MAJIRA YA
SAA 20:15HRS USIKU KATIKA MTAA WA NYASAKA KATA YA NYASAKA WILAYA YA
ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KALA
MACHAGE MIAKA 66, MKAZI WA MTAA WA NYASAKA ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MJUKUU WAKE JINA
TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 16, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI
SHULE YA SEKONDARI NYASAKA, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.
INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA
AKIISHI NA MJUKUU WAKE NYUMBANI KWAKE TOKEA MWAKA 2011 AKITOKEA MUSOMA
VIJIJINI, INASEMEKANA KUWA KWA KIPINDI CHOTE HICHO MTUHUMIWA ALIKUA NA
TABIA YA KUMFANYIA UKATILI MJUKUU WAKE KWA KUMWINGILIA KIMWILI WAKATI
AMBAPO MKEWE HAYUPO HUKU AKIMTISHIA KUWA ENDAPO ATASEMA BASI
ATAMUACHISHA SHULE KISHA ATAMRUDISHA KIJIJINI KWAO.
INASEMEKANA KUWA BINTI
ALIENDELEA KUVUMILIA HALI HIYO BILA KUMWAMBIA MTU YEYOTE, NDIPO TAREHE
TAJWA HAPO JUU WAALIMU WALITILIA MASHAKA HALI YAKE YA KIAFYA NDIPO
WALIMPELKA HOSPITALI KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI, NDIPO BAADA YA
UCHUNGUZI BINTI ALIGUNDULIKA KUWA ANAUJAUZITO WA MIEZI MINNE NA
ALIPOHOJIWA ALIDAIWA KUWA AMEPEWA NA BABU YAKE.
WAALIMU WALITOA TAARIFA POLISI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA
NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA, MTUHUMIWA YUPO POLISI KWA MAHOJIANO
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA
KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA BAADHI YA WATU
WENYE TABIA YA KUWATAMANI KIMAPENZI WANAFUNZI KWA KUWARUBUNI AIDHA KWA
FEDHA ZAO KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA, PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUTOA
TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA ZA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA
NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment